MFUKO WA AFYA NA TIBA

Mfuko wa Afya na tiba umeanzishwa kwa lengo la kumwezesha Mwanachama kuweka akiba kila mwezi ili fedha hizo zimsaidie kuwahudumia wategemezi kama vile wazazi, yatima, wasaidizi wa nyumbani na watoto wa mwanachama ambao wana umri zaidi ya miaka 18 ambapo Sera ya matibabu ya Mwajiri haitoi huduma hiyo. 

Faida za kujiunga na Mfuko huu

  • Mfuko huu utazaa riba juu ya akiba kama ilivyobainishwa kwenye Sera ya hisa na Akiba.
  •    Huduma ya Afya itatolewa kwa kuzingatia kiwango cha michango ya Mwanachama na huduma hii haitatolewa zaidi ya mara mbili ya akiba ya Afya ya Mwanachama (Afya Savings).

  •      Riba itakuwa ni asilimia moja (1%) kwa mwezi katika salio.

  •        Kipindi cha marejesho ya mkopo huu hakitazidi miezi kumi na nane (18).

Jinsi ya kujiunga na Mfuko wa Afya na Tiba

  • Mwanachama atahitajika kujaza fomu ya maombi ya kujiunga na huduma hii.

  • Kiwango cha chini cha uchangiaji kwa akiba ya afya na Tiba kwa mwezi kitakuwa ni shilingi 30,000/= Aidha, mwanachama yuko huru kuchangia zaidi ya kiwango hicho kulingana na uwezo na mahitaji yake ya kugharamia afya na tiba.

  • Mwanachama atachangia kwa kukatwa kwenye mshahara wake wa kila mwezi.