MFUKO WA RAMBIRAMBI

Mfuko wa Rambi Rambi umeanzishwa kwa lengo la kumjengea mwanachama tabia ya kuweka akiba mara kwa mara ili fedha hizo zimsaidie kukidhi mahitaji na gharama zitakazohitajika endapo atapatwa na msiba. Walengwa wa huduma hii ni mme/mke wa mwanachama/watoto/mama/baba pamoja na wakwe.

Faida za kujiunga na Mfuko huu

  • Huduma hii ya rambi rambi itatolewa kwa mlengwa mara baada ya kujiunga na Chama.

  • Mwanachama atapewa rambi rambi kiasi cha TZS 750,000/= baada ya kutimiza masharti yaliyotajwa hapo chini.

  • Kiwango cha rambirambi kinaweza kubadilika kulingana na idadi ya wanachama watakaojiunga na mfuko huu.

Jinsi ya kujiunga na Mfuko wa Rambi Rambi

  • Mwanachama atakuwa amejiunga kwenye mfuko huu mara baada ya kuanza kuchangia na kuthibitishwa kuwa Mwanachama kamili kama ilivyoainishwa kwenye Katiba ya Chama.

  • Mwanachama atakuwa anachangia kiasi cha TZS 5,000/= kila mwezi baada ya kujiunga na Chama.

  • Mwanachama atachangia kwa kukatwa kwenye mshahara wake wa kila mwezi.