Mfuko wa Elimu

Mfuko wa Elimu umeanzishwa kwa lengo la kumjengea Mwanachama tabia ya kuweka akiba mara kwa mara ili baadaye atumie fedha hizo katika kulipa Karo/ada za shule na vyuo yeye binafsi, watoto wake au mwana familia yeyote ambaye ni mtegemezi wa Mwanachama.

Faida za kujiunga na Mfuko huu

  • Mfuko huu utazaa riba juu ya akiba kama ilivyobainishwa kwenye Sera ya hisa na Akiba.

  • Mfuko wa Elimu utatolewa kwa kuzingatia kiwango cha michango ya mwanachama na hautatolewa zaidi ya mara mbili ya akiba ya Elimu ya Mwanachama (Education Savings)

  • Riba itakuwa ni 1% kwa mwezi katika salio

  • Kipindi cha marejesho cha mkopo huu hakitazidi miezi kumi na nane (18);

  • Mwanachama anayechangia mfuko huu endapo atakuwa hana salio la mkopo wa elimu ataruhusiwa kuchukua michango yake isiyozidi kiwango cha asilimia hamsini (50%) kwa ajili ya matumizi yake mengine na ataruhusiwa kufanya hivyo mara mbili tu kwa mwaka.

Jinsi ya kujiunga na Mfuko wa Elimu

  • Mwanachama atahitajika kujaza fomu ya maombi ya kujiunga na Bidhaa Mpya .

  • Kiwango cha chini cha uchangiaji kwa akiba ya elimu kwa mwezi kitakuwa ni shilingi elfu thelathini tu (30,000/=) lakini mwanachama yuko huru kuchangia zaidi ya kiwango hicho kulingana na uwezo na mahitaji yake ya kugharamia elimu.

  • Mwanachama atachangia kwa kukatwa kwenye mshahara wake wa kila mwezi.