MKOPO WA PAPO KWA PAPO

Huduma hii inalenga kumwezesha Mwanachama kupata mkopo wa dharura na kwa haraka zaidi ili kukidhi mahitaji muhimu yanayojitokeza ghafla bila kutegemea.

Faida za Huduma ya Papo kwa Papo

  • Mkopo huu hauchangiwi;

  • Mwanachama ataweza kupatiwa mkopo kuanzia kiwango cha TZS 50,000 hadi TZS 2,000,000;

  • Mkopo huu hutolewa ndani ya Masaa 24;

  • Kipindi cha marejesho cha mkopo huu hakitazidi miezi minne (4);

  • Riba itayotozwa ni 1%  kwa mwezi;

  • Mkopo huu hauhitaji wadhamini;

Jinsi ya kupata huduma hii

  • Mwanachama atahitajika kujaza fomu ya maombi ya mkopo wa Papo kwa Papo

  • Marejesho ya mkopo yatatokana na makato kutoka kwenye mshahara wa mwanachama. Endapo Mwanachama atahitaji kulipa mkopo kupitia vyanzo vingine na kabla ya tarehe ya mishahara, ataruhusiwa kufanya hivyo