MFUKO WA KUSTAAFU

Mfuko wa Kustaafu umeanzishwa kwa lengo la kumjengea tabia mwanachama ambaye ni ‘mstaafu mtarajiwa’ kujiwekea akiba mara kwa mara ili zimsaidie kutatua matatizo yake baada ya kustaafu, kuacha au kuachishwa kazi kutoka katika ajira ya Mamlaka ya Mapato Tanzania. Akiba hii itamsaidia Mwanachama ambaye amestaafu kuendeleza maisha bora na yenye afya njema .

Faida za kujiunga na Mfuko huu

  • Mfuko huu utazaa faida ya asilimia kumi (10%) kwa mwaka kwa kiwango kinachoanzia TZS 500,000;

  • Mwanachama atapatiwa akiba zake zote ikiwemo faida itakayopatikana baada ya kustaafu, kuacha au kuachishwa kazi kutoka katika ajira ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.

  • Mwanachama anayechangia mfuko huu atapata fursa ya kuhudhuria warsha na semina mbalimbali za Ujasiriamali ambazo zitakuwa zikiandaliwa kila mwaka

Jinsi ya kujiunga na Mfuko wa Kustaafu

  • Mwanachama atahitajika kujaza fomu ya maombi ya kujiunga na huduma hii.

  • Kiwango cha chini cha uchangiaji kwa akiba ya kustaafu kwa mwezi kitakuwa ni shilingi elfu ishirini (30,000/=). Aidha, mwanachama yuko huru kuchangia zaidi ya kiwango hicho kulingana na uwezo na mahitaji yake ya baadaye.

  • Mwanachama atachangia kwa kukatwa kwenye mshahara wake wa kila mwezi.