Akiba ya Lazima

Ni sehemu ya fedha ambazo mwanachama atakuwa anachangia kwa kuwekeza kwenye Chama ili zimpe uwezo wa kukopa pale inapohitajika

Faida za kuweka Akiba

  • Humwezesha mwanachama kujenga tabia ya kuweka akiba mara kwa mara ili zimsaidie baadaye;

  • Sehemu ya Kiwango cha Akiba za mwanachama hutumika kama dhamana endapo mwanachama akikopa

  • Husaidia mwanachama kupanga vizuri mapato na matumizi kwa kuweka akiba mara kwa mara;

  • Husaidia kujenga mtaji wa mwanachama

  • Kiwango cha chini cha kuchangia mfuko huu wa Akiba ni shilingi elfu ishirini tu (30,000/=) kwa mwezi. Aidha mwanachama anaweza kuweka zaidi ya kiwango hiki kulingana na uwezo na mahitaji yake.