Rambirambi ni huduma ambayo kila mwanachama huchangia Tzs. 10,000 kila mwezi kwenye mfuko wa rambirambi kwa lengo la kuwahudumia Wanachama pale wanapofariki au kufiwa na wategemezi wao kama ilivyoainishwa katika sera ya Rambirambi ambapo mwanachama hupewa kiasi cha TZS. 1,500,000/= kama pole ya msiba na kumsaidia mwanachama wakati wa msiba huo.
Faida na namna Huduma ya Rambirambi inavyotolewa
- Kila mwanachama anastahili kupata huduma hii baada ya kujiunga na kuanza kuchangia kiasi cha TZS. 10,000
- Kila mwanachama atapewa kiasi cha TZS. 1,500,000 pale apatwapo na msiba
- Kiasi cha kuchangia kinaweza kubadilika kulingana na maamuzi yaliyopitishwa na Mkutano Mkuu na hali ya soko la fedha kwa wakati husika
- Mwanachama anaweza kuchangia katika Akaunti hii kila anapopata fedha (Kwa njia ya Mshahara au Kuweka fedha katika akaunti za chama au Makubaliano ya Bank Standing Order).
Walengwa wa huduma ya Rambirambi
Huduma ya rambirambi itahusisha mwanachama na wategemezi wa mwanachama kama ifuatavyo;
- Wazazi wawili wa Mwanachama
- Wakwe wawili wa Mwanachama
- Mwenza wa Mwanachama
- Watoto wa Mwanachama
Masharti ya Kupata Huduma ya Rambirambi
- Mwanachama atawasilisha kwenye Chama taarifa za wategemezi wake kwa kujaza fomu iliyopo kwenye tovuti ya Chama (Fomu Namba A) kisha kuituma kwenye email ya Chama. (Bofya maneno haya kujaza fomu)
- Mwanachama anatakiwa kuhuisha taarifa za wategemezi wake kila mara inapotokea mabadiliko ya wategemezi wake.
- Mwanachama hatalipwa rambirambi endapo hachangii au anadaiwa limbikizo lolote la mchango kabla ya janga la kifo kutokea.
- Mwanachama hatanufaika zaidi ya mara moja katika kila nafasi ya mtegemezi isipokuwa kwa nafasi ya mtoto.
- Taarifa ya kifo itawasilishwa na Mwenyekiti wa Kituo husika kwa Meneja wa Chama kwa njia rasmi ya mawasiliano. Chama kinaweza kujiridhisha kwa njia mbalimbali juu ya taarifa ya kifo iliyowasilishwa na mwanachama, ikiwemo kuwasiliana na kuomba uthibitisho kutoka Idara ya Rasilimali Watu, Makao Makuu ya TRA