MASWALI NA SULUHISHO LA MASWALI

NA

MASWALI

JIBU

1.

Naomba kujua utaratibu wa kujiunga na chama

  1. Kujaza fomu ya uanachama (TRASACCO-1b      Version 2)
  2. Kulipa ada ya kiingilio TSH 50,000.00 katika benki akaunti ya chama (CRDB 0111328947801)
  3. Kulipia HISA 30 zenye thamani ya TSH 600,000.00 kupitia benki akaunti ya chama (CRDB 0111328947801). Unaweza kulipa HISA kwa awamu au kwa Mkupuo
  4. Tuma risiti za malipo kwa barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
  5. Kuwasilisha fomu zilizojazwa kwa ukamilifu kwenye ofisi za Chama kwa mfumo wa kielectroniki au kwa mkono.
  6. Ambatanisha picha mbili za passport size.

2

Je mtu akishajiunga na chama itachukua muda gani kupata mkopo?

  1. Kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika namba 6 ya mwaka 2013 Kifungu cha 41 (1) pamoja na Sera ya Mikopo, sehemu ya pili, kipengele cha 2.1.1.3 Mwanachama mpya atapata stahili ya kuomba mkopo mara baada ya kulipa kiingilio,kukamilisha angalau nusu ya Hisa za lazima na ameshaanza kukatwa michango ya akiba ya kila mwezi kutoka kwenye mshahara wake angalau kwa kipindi kisichopungua miezi miwili (2).
  2. Kipengele cha 2.1.1.4 cha Sera ya Mikopo kinaeleza kuwa Mwanachama ambaye ni mwajiriwa mpya wa Mamlaka ya Mapato atapata stahili ya kuomba mkopo baada ya kutimiza masharti ya kipengele 2.1.1.3 hapo juu na kwamba kipindi cha marejesho ya mkopo kisizidi kipindi chake cha  majaribio (Probation period) ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania.

3

Naomba kujua Akiba zangu ni kiasi gani?

Mwanachama  anaweza kupata taarifa zake kwa kuingia kwenye website ya TRA SACCOS (Members Portal) ataweza kuona salio la mkopo wake kwenye stetiment yake kwa kutumia nywila (password na user name) itakayomwezesha kuingia kwenye account yake.

Hivyo basi Mwanachama anatakiwa atumie Members portal ili kupata taarifa zake.

4

Naomba kujua mwanachama akiomba mkopo,mkopo wake unachukua muda gani kukamilika na pesa kuwekwa kwenye Account?

Kwa wastani malipo ya mikopo ufanyika kama ifuatavyo:

  1. Mkopo wa Papo2Papo  huchukua  siku 1
  2. Mkopo wa Dharura siku 3; ila kama kiasi cha mkopo hakizidi 2,000,000/=, inachukua siku 1
  3. Mkopo wa Maendeleo ya Jamii huchukua hadi  siku 7
  4. Mkopo wa Elimu  huchukua siku 5

NB: Ikumbukwe kwamba Mwanachama ana wajibu kuhakikisha anakamisha kujaza offer ya mkopo husika, mkataba wa mkopo pamoja na fomu mbili za wadhamini na kisha kuzirejesha ama kwa mfumo laini ama kwa kuzileta fomu halisi katika ofisi za chama kuwezesha mchakato wa kutoa mkopo huo

5

Kiasi cha juu cha mkopo ni shilling ngapi? Na muda  wa mwisho wa marejesho miaka mingapi?

  1. Mkopo wa Papo2papo kiwango cha juu ni sh. 2,000,000 (Muda wa marejesho ni miezi 2).
  2. Mkopo wa Dharura kiwango cha juu ni sh. 5,000,000 muda wa marejesho ni miezi 6
  3. Mkopo wa Maendeleo ya Jamii ni mara 3 ya akiba za mwanachama ila isizidi milioni 150 (Sh150,000,000) kwa kuzingatia uwezo wa mshahara, Muda wa marejesho ni miezi 60 (Miaka 5)
  4. Mkopo wa Elimu ni mara 2 ya akiba ya elimu, Marejesho ni miezi 18

6

Je naweza kukopa hata bila kuwa na michango?

  1. Anayeruhusiwa kukopa ni Mwanachama hai
  2. Kwa mkopo wa Papo kwa Papo na Dharura mwanachama anaweza kukopa pasipo kuangalia kiasi cha akiba alichonacho kwenye Chama.
  3. Kwa mkopo wa Maendeleo ya Jamii, mwanachama atakopeshwa kiasi cha mkopo kisichozidi mara 3 ya akiba zake
  4. Kwa mkopo wa Elimu na Afya, mwanachama atakopeshwa kiasi cha mkopo kisichozidi mara 2 ya akiba zake kwenye mfuko husika.

7

Mkopo wangu umebaki kiasi gani?

Chama kimezindua mfumo laini kwa kutumia “members portal “ambapo wanachama wanaweza kuingia kwenye mtandao na kupata taarifa zake.

Mwanachama akiingia kwenye website ya TRA SACCOS (Members Portal) ataweza kuona salio la mkopo wake kwenye stetiment yake

8

Naweza kufanya Top up? Kama ndio, ni kiasi gani?

  1. Marejesho ya mkopo unaoendelea  yawe yamekwisha katwa kwa mfululizo wa kipindi cha miezi sita tangu mkopo huo utolewe bila kukosa.
  2. Mkopo huo ni lazima uwe ni wa Maendeleo ya jamii
  3. Kiwango cha marejesho ya mkopo mpya ni lazima kilingane na kiwango kilichokuwepo au kuzidi
  4. Kiasi cha Top up ni tofauti kati ya akiba mara 3 na salio la mkopo (principal) kwa kuzingatia uwezo wa mshahara

9

Baada ya kukamilisha mikataba pamoja na ofa je malipo yatachukua muda gani kuingizwa kwenye akaunti ya mwanachama?

Ndani ya siku 2

11

Je naweza kupunguza /kuchukua sehemu ya akiba zangu kidogo badala ya kukopa?

  1. Kwa mujibu wa Sera ya Hisa na Akiba kipengele cha 4.2.7 Akiba za lazima haziwezi kurejeshwa au kupunguzwa kwa Mwanachama isipokuwa tu uanachama unapokoma.
  2. Akiba za hiari kama ya Elimu,Wastaafu na akiba ya Afya inaruhusiwa kurejeshwa kwa Mwanachama bila hata uanachama wake kukoma, kwa kuzingatia  Sera ya Hisa na Akiba, kipengele namba  4.2 na 4.3

12

Naomba kujua jinsi ya kukokotoa riba ya Mkopo wangu..

Riba hukokotolewa kwa kutumia mfumo wa PROSACCO kwa kutumia njia zifuatazo

  1. Papo2papo ni 1% kwa mwezi kwa mstari mnyoofu (Straight line Method)

2.Dharura ni 1% kwa mwezi kwa mstari mnyoofu (Straight line Method)

  1. Maendeleo ya Jamii ni 10% kwa mwaka kwenye salio la mkopo (Reducing balance method)
  2. Elimu ni 1% kwa mwezi kwa mstari mnyoofu(Straight line Method)

13

Naweza kujua makato /marejesho kwa mwezi ya mkopo kiasi fulani kwa muda fulani?

Mwanachama ataweza kujua mwenendo wa malipo yake ya mkopo kwa kuangalia kwenye jedwali la ulipaji wa mkopo (Loan repayment schedule). Jedwali hili lina taarifa za kiasi cha Mkopo ulioomba,Makato kwa Mwezi,muda wa marejesho na kiasi cha riba katika kila rejesho kulingana na aina ya Mkopo.

14

Naomba  kupewa utaratibu wa kupata mkopo?

  1. Lazima kwanza muombaji wa mkopo awe Mwanachama hai wa TRA SACCOS
  2. Kujaza kikamilifu fomu husika ya maombi ya mkopo
  3. Kuwasilisha fomu ya maombi kwenye ofisi za Chama
  4. Kusaini ofa ya mkopo baada ya kamati ya mikopo kuidhinisha, isipokuwa kwa mkopo wa papo kwa papo ambao hauhitaji kusaini offer.
  5. Kusaini mikataba ya mkopo baada ya kamati ya mikopo kuidhinisha, isipokuwa kwa mkopo wa Papo kwa Papo na dharura na kuiwasilisha kwenye ofisi ya Chama
  6. Kuandikiwa cheki na kupelekwa benki kwa ajili ya kuingiziwa fedha ya mkopo kwenye akaunti

15

Je naruhusiwa  kupunguza Mkopo?

Ndiyo.

Mwanachama anayetaka kupunguza DENI kwa kulipa sehemu ya mkopo alionao katika Chama, atatakiwa kuandika barua ya kusudio hilo kwa Mwenyekiti wa Chama na katika barua hiyo atataja kiasi ambacho anataka kulipa kisha ataruhusiwa kufanya hivyo na atapewa nambari ya akaunti ambayo atatakiwa kuingiza fedha hizo benki na kisha kuwasilisha Hati ya Malipo katika ofisi za Chama.

Kwa Mwanachama anayelipa kwa mkupuo kupunguza deni la mkopo, atahitajika kulipa mkopo halisi bila riba endapo kipindi cha marejesho kilichosalia ni zaidi ya mwaka mmoja; chini ya muda huo atalipa mkopo halisi na riba yake

16

Je naweza kulipa mkopo wote kwa mkupuo na utaratibu ukoje?

Ndiyo.

  1. Mwanachama atatakiwa kuandika barua ya kusudio la kulipa kwa Mwenyekiti wa Chama
  2.  Mkuu wa idara ya mikopo au Afisa Mikopo atakokotoa kiasi cha deni lililosalia
  3. Mwanachama ataruhusiwa kufanya hivyo na atapewa nambari ya akaunti ambayo atatakiwa kuingiza fedha hizo benki
  4. Mwanachama atalipa mkopo uliosalia bila riba yake (endapo mkopo umekuwa ukirejeshwa kama ilivyo kwenye jedwali la mkopo)
  5. Mkopo wa Papo kwa Papo hulipwa na riba yake yote
  6. Mwanachama atawasilisha Hati ya Malipo katika ofisi za Chama.

17

Naomba kujua taratibu za kununua madeni ya mikopo ya taasisi nyingine?

 Utaratibu ni kwamba Mwanachama hutembelea ofisi za SACCOS na kueleza nia yake ya kulipa Mkopo alionao kutoka Taasisi nyingine,kisha Afisa mkopo hukokotoa uwezo wa Mkopo ambao mwanachama atakuwa na uwezo wa kuulipa kisha hushauriwa kuleta uthibitisho wa Bakaa ya Mkopo alionao kutoka Taasisi nyingine.Kisha taratibu nyingine hufuata.Ikumbukwe kuwa wajibu wa chama ni kumsaidia Mwanachama kwa kumpa ushauri na namna ambayo atalipia Mkopo mwingine kwa kuchukua Mkopo kutoka SACCOS.

18

Je naweza KUKOPA mkopo kwa kutegemea marejesho yatokanayo na vyanzo vingine vya mapato mbali na mshahara?

Hapana.

  1. Marejesho ya mkopo yatafanyika kila mwisho wa mwezi na yatakatwa kupitia kwenye mshahara wa mwanachama. Hivyo wakati wa kumfanyia mwanachama mahesabu ya mkopo, uwezo wa kurejesha utazingatia mshahara tu.
  2. Hakikisha kuwa slip ya mshahara ni ya mwezi huo (current) na kama hazijatoka slip iwe ya mwezi uliopita.
  3. Kabla ya kuangalia salio la mshahara (net salary), lazima uangalie na kuzingatia component ya Mshahara ambao ni basic salary.

19

Je, uki deposit akiba benki inachukua  muda gani kuomba kukopa?

Mwanachama ataruhusiwa kuomba mkopo endapo

1.Atakuwa amelipia kiingilio, amelipia asilimia 50% ya hisa za uanachama na pia atakuwa amechangia chama kwa muda usiopungua miezi miwili.(Rejea majibu ya swali namba1 )

20

Je, nikiacha ajira kwenye Mamlaka ya Mapato Tanzania, na ikawa mkopo wangu haujaisha, nitatakiwa kufanya nini?

  1. Kuandika barua kukijulisha chama juu ya kuacha/kuachishwa kazi na kueleza namna utakavyoendelea kuhudumia Mkopo wako hadi utakapo isha.
  2. Kulipa mkopo wote kwa mkupuo kama inawezekana
  3. Kutoa taarifa juu ya mahali utakapokuwa unafanyakazi / ishi /biashara.

21

Kwa nini riba juu ya akiba huilipwi mapema (mwanzoni mwa mwaka)?

  1. Riba hulipwa baada ya kuandaa hesabu za Mwaka za Chama ambazo huwa zinahitajika ndani ya miezi mitatu tangu mwaka wa fedha kuisha kwa Mujibu wa Sheria ya Ushirika ya 2013.Hivyo basi wakati wa upitishaji wa hesabu hizo hapo ndo Bodi pia hupitisha riba juu ya akiba na Hulipwa kila baada ya tarehe 30 Machi kila mwaka.

24

Kwa nini ninatakiwa kuwa na wadhamini wa mkopo wakati tayari chama kinakata bima kwenye mkopo wangu? Je Bima inatumika wapi?

  1. Kuwa na mdhamini wa mkopo ni hitaji la kisheria
  2. Kazi ya Bima ya Mkopo kwa mujibu wa Sera ya Mikopo ni Kinga  dhidi ya bakaa ya Mikopo itakayokua imeachwa na wanachama waliofikwa na aidha mauti/kufariki au Mwanachama aliepatwa na ulemavu wa kudumu na kushindwa kufanya kazi.
  3. Pale mwanachama anaposhindwa kurejesha mkopo kwa sababu zingine tofauti na hizo za kipengele  na. 2 juu, mdhamini anawajibika kusaidia kufanikisha marejesho ya mkopo huo.

25

Kwa nini kuwa na wadhamini wa mkopo wakati mwajiri ndiye mdhamini wangu?

  1. Kuwa na mdhamini wa mkopo ni hitaji la kisheria
  2. Mwajiri siyo mdhamini wa wanachama bali ni mlezi wa chama

Kwa msaada na maswali zaidi wasiliana nasi