Aina hii ya mkopo inatolewa kwa mwanachama hai wakati wowote itokeapo dharura. Kama jina la mkopo huu linavyojieleza, aina hii ya mkopo itatolewa kwa mwanachama aliyepatwa na dharura (emergency) tu kwa ajili ya kumsaidia kwa wakati husika

  • Kiwango cha juu cha mkopo wa dharura hakitazidi shilingi milioni nane (8,000,000/=)
  • Muda wa marejesho hautazidi miezi 12
  • Kiwango cha riba ni asilimia moja (1%) kwa mwezi (Straight Line method)

Matukio yafuatayo yanaweza kuwa ni ya dharura kwa mwanachama

  • Kupata msiba wa karibu wa familia ya mwanachama
  • Tatizo la kuugua au kuuguliwa na mwanafamilia
  • Mgogoro baina ya mwenye nyumba na mpangaji utakaopelekea mpangaji (mwanachama) kutaka kuondolewa katika nyumba hivyo kuhitaji fedha za haraka kwa ajili ya pango mpya
  • Kulipa karo ya mtoto wa mwanachama ambaye yu karibu kusimamishwa masomo.
  • Mwanachama kuibiwa, kuvunjiwa nyumba (Theft and Bulglary) na kuungua nyumba au kuteketezwa kwa moto
  • Dharura zingine ambazo Bodi kupitia kamati ya Mikopo itaridhika na kuthibitisha kuwa ni miongoni mwa dharura

Utaratibu wa Mkopo wa Dharura

  • Mwanachama hataruhusiwa kupata mkopo mwingine wa dharura endapo hatakuwa amekamilisha marejesho ya mkopo wa dhararu uliotangulia
  • Mwanachama anaweza kukopa mkopo wa dharura hata kama ana mkopo mwingine kama vile mkopo wa maendeleo ya jamii.
  • Mwombaji atahitajika kujaza fomu ya maombi (TRASACCO-2) na kuiwasilisha kwa Mwenyekiti wa chama
  • Dhamana ya mkopo wa dharura kwa mwanachama aliye ndani ya ajira ni hisa, akiba alizonazo, pensheni yake na wadhamini wawili (2)
  • Dhamana ya mkopo kwa mwanachama aliye nje ya ajira ni hisa, akiba alizonazo, wadhamini wawili (2) ambao ni waajiriwa wa Mamlaka ya Mapato au mali nyinginezo zisizohamishika anazomiliki mwanachama

Jinsi ya Kuomba