Utaratibu wa Mkopo wa JIPANGE
- Mkopo huu unatolewa kwa mwanachama mwenye akaunti za Wastaafu au/na Wekeza
- Kiwango cha juu cha mkopo ni milioni hamsini (50,000,000.00) lakini si zaidi ya mara mbili ya jumla ya akiba ya wastaafu na wekeza
- Muda wa marejesho hautazidi miaka mitatu(3) yaani miezi 36 na marejesho yatategemea uwezo wa kulipa kwa kutumia makato kutokana na mshahara pasipo kuathiri sheria mbalimbali zilizopo ambazo zinambana mkopeshaji na mkopaji
- Dhamana ya mkopo kwa mwanachama aliye ndani ya ajira ni hisa, akiba alizonazo, pensheni yake na wadhamini wawili (2)
- Dhamana ya mkopo kwa mwanachama aliye nje ya ajira ni hisa, akiba alizonazo, wadhamini wawili (2) au mali nyinginezo zisizohamishika anazomiliki mwanachama
- Riba ni asilimia kumi na mbili (12%) kwa mwaka katika salio (Reducing Balance Method)
- Mkopaji anaweza kupewa mkopo mwingine (TOP UP) ikiwa marejesho sita(6) ya mkopo wa awali yameshafanyika.
Jinsi ya Kuomba Mkopo