Mkopo wa Maendeleo ya Jamii (SDL) unatolewa kwa lengo la kumsaidi mwanachama katika kukidhi mahijati yake ya kijamii kama vile;
- Karo za shule/Chuo
- Ununuzi wa samani (Furniture)
- Ujenzi na umilikaji wa nyumba
- Ununuzi wa vyombo vya moto
- Mtaji kwa ajili ya biashara mbalimbali
- Mahitaji mengine yanayofanana na hayo yaliyotajwa hapo juu
Utaratibu wa Mkopo wa Maendeleo ya Jamii
- Mkopo huu unatolewa kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya muda mrefu ya mwanachama
- Kiwango cha juu cha mkopo ni mara tatu ya akiba ya mwanachama
- Muda wa marejesho hautazidi miaka mitano(5) yaani miezi 60 na marejesho yatategemea uwezo wa kulipa kwa kutumia makato kutokana na mshahara pasipo kuathiri sheria mbalimbali zilizopo ambazo zinambana mkopeshaji na mkopaji
- Dhamana ya mkopo kwa mwanachama aliye ndani ya ajira ni hisa, akiba alizonazo, pensheni yake na wadhamini wawili (2)
- Dhamana ya mkopo kwa mwanachama aliye nje ya ajira ni hisa, akiba alizonazo, wadhamini wawili (2) au mali nyinginezo zisizohamishika anazomiliki mwanachama
- Riba ni asilimia tisa (9%) kwa mwaka katika salio (Reducing Balance Method)
- Mkopaji anaweza kupewa mkopo mwingine (TOP UP) ikiwa marejesho sita(6) ya mkopo wa awali yameshafanyika.
Jinsi ya Kuomba Mkopo