TRA SACCOS
Home Resources News Article

TRA SACCOS YASHIRIKI JUKWAA LA WADAU WA SEKTA YA FEDHA NCHINI

Published on Apr 11, 2026

TRA SACCOS, kupitia Mwenyekiti wake, CPA Mbogo Kerenge, imeshiriki katika Jukwaa la Wadau wa Sekta ya Fedha nchini lililoandaliwa na kuratibiwa na Wizara ya Fedha.

Jukwaa hilo lilijikita katika kujadili utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa miaka kumi (2020/21–2029/30), chini ya kauli mbiu inayosema: “Sekta ya Fedha Bunifu na Yenye Uwajibikaji kwa Maendeleo Endelevu na Jumuishi ya Jamii na Uchumi.”

Kushiriki katika jukwaa hilo kumempa TRA SACCOS fursa ya kupanua uelewa wake, kubadilishana uzoefu na wadau wengine wa sekta, pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kimkakati. Vilevile, imepata nafasi ya kuwasilisha mchango wake katika kuendeleza sekta ya ushirika wa kifedha, hususan katika kuwawezesha wanachama kupata huduma za kifedha bora, salama na endelevu.

Hatua hii inaonyesha dhamira thabiti ya TRA SACCOS katika kuimarisha sekta ya fedha jumuishi na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa

Mwenyekiti CPA Mbogo Kerenge akichangia mada katika jukwaa la wadau wa fedha.
View Full Image
View Full Image
View Full Image