Home
Loan Product
MKOPO WA DHAMANA YA HATIFUNGANI (BOND LOAN)
Overview
Je, unamiliki Hatifungani za Serikali au Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na unahitaji fedha kwa ajili ya mradi, biashara, elimu au mahitaji mengine muhimu?
Bond Loan ni bidhaa ya mkopo inayolenga kuwapa wanachama wanaomiliki hatifungani za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) fursa ya kupata fedha bila kulazimika kuuza au kuondoa uwekezaji wao kwenye hatifungani hizo. Bidhaa hii inalenga kumwongezea mwanachama wigo wa kupata mikopo bila kulazimika kurejesha mikopo hiyo kwa njia ya mshahara. Hii ni fursa kwa wanachama kustawisha uchumi wao na hivyo kuwawezesha kutatua changamoto mbalimbali za kiuchumi, kuongeza uwekezaji katika mitaji ya soko la fedha au aina nyingine za uwekezaji.
Sifa na Vigezo vya Bond Loan
- Kiwango cha juu cha mkopo: TZS 80,000,000 ambapo mwanachama anaweza kutumia hatifungani tofauti tofauti zinazotolewa na Benki Kuu (BOT) kama dhamana ya mkopo huu.
- Riba: 9% kwa mwaka kwa mfumo wa salio linalopungua (Reducing Balance Method).
- Muda wa marejesho ni hadi miaka mitano (5), sawa na miezi 60 na marejesho yatategemea thamani ya malipo ya coupon (riba) inayotokana na hatifungani iliyowekwa dhamana kwa ajili ya mkopo huu
- Dhamana: Hatifungani ya Serikali au BoT.
- Mpangilio wa marejesho huzingatia mapato ya riba (coupon) yanayotokana na Hatifungani iliyowekwa kama dhamana.
Utaratibu wa Utoaji wa Bond Loan
- Pakua fomu ya Bond Loan kwenye tovuti ya chama na ujaze kwa usahihi.
- Ambatanisha nyaraka zote muhimu zinazohitajika kuthibitisha umiliki wa Hatifungani na utambulisho wako.
- Wasilisha fomu iliyokamilika katika ofisi za TRA SACCOS au kwa barua pepe rasmi iliyoainishwa.
- Baada ya kupokea maombi, fomu itahakikiwa kwa mujibu wa taratibu zake. Maombi yatakapokidhi vigezo vilivyowekwa, mkopo utatolewa kwa mwanachama.
Get In Touch
Do you want to join TRA SACCOS, need to apply for this product, or have an enquiry? Reach out to us and our team will be happy to assist you.