Home
Loan Product
Mkopo wa Week-End
Overview
Ni mkopo wa kidijitali unaopatikana muda wote (24/7) kwa wanachama kwa riba ya 5%, bila dhamana na kiwango cha juu cha TZS 200,000. Na pesa huingizwa ndani ya sekunde kupitia App ya "TRA SACCOS Kiganjani" au USSD *150*45#.
1.0 Mkopo wa Week-End (Mkopo kwa Sekunde)
Mkopo wa Weekend unapatikana kwa njia ya mtandao muda wote/masaa ishirini na nne. Mkopo huu una sifa zifuatazo:
- Mwanachama anapata mkopo ndani ya Sekunde baada ya kufanya maombi
- Kiwango cha juu cha mkopo ni TSH 200,000.00
- Riba ya mkopo ni asilimia tano (5%); Mfano: kama mwanachama ameomba shilingi laki mbili, atalipa TSH 210,000.00
- Muda wa marejesho hautazidi siku therathini (30) baada ya kuomba mkopo.
- Mkopo huu hauhitaji dhamana yeyote
- Mwanachama atalazimika kulipa adhabu ya asilimia tano (5%) kwa kila mwezi anaochelewesha malipo
1.2 Vigezo na Masharti
- Mwanachama atakaepitiliza muda wa marejesho (Siku 30) atapata adhabu ikiwa ni pamoja na kufungiwa kutumia huduma hii kwa muda wa miezi mitatu.
- Mwanachama hataweza kupata mkopo mpya endapo bado ana deni la mkopo huu au aina nyingine ya mkopo
1.3 Kujiunga na Huduma za mtandaoni
Ili mwanachama aweze kuomba mkopo huu atatakiwa kujiunga na huduma za mtandaoni kwa kufuata utaratibu ufuatao:
- Mwanachama ataomba kuwezeshwa kujiunga na huduma za mtandaoni kwa kujaza fomu JIKIMU ambayo ipo kwenye tovuti yetu.
- Mwanachama atatakiwa kutuma fomu hii kwa kutumia email yake ya TRA (...@tra.go.tz) to info@trasaccos.co.tz
Get In Touch
Do you want to join TRA SACCOS, need to apply for this product, or have an enquiry? Reach out to us and our team will be happy to assist you.