Akiba ya AFYA ni akaunti ya akiba ambayo inamuwezesha mwanachama kuchangia kwa hiari yake mwenyewe ili kukidhi changamoto ya kiafya ambayo inaweza kujitokeza kwake mwenyewe, ndugu au wategemezi wake kwa kujaza fomu maalum ya kujiunga na bidhaa hii inayopatika kwenye tovuti au ofisi ya Chama.

      Faida za Akiba ya Afya

  1. Kiwango cha chini cha kuweka ni TZS. 50,000
  2. Akiba ya Afya itazaa faida ya riba juu ya akiba (Interest on Savings) kila Mwaka.
  3. Akiba ya Afya inakuwezesha kupata Mkopo wa Afya ambao ni mara mbili (2) ya Akiba ya Afya.
  4. Malipo hufanyika ndani ya masaa 24 endapo mwanachama akitaka kupunguza kiasi cha Akiba ya Afya kwa njia ya Simu au Benki.
  5. Mwanachama anaweza kuchangia katika Akaunti hii kila anapopata fedha (Kwa njia ya Mshahara au Kuweka fedha katika akaunti za chama au Makubaliano ya Bank Standing Order).

 

Akaunti za Benki za Chama

Jina la Akaunti ni: TRA SACCOS LTD:

  • NBC 012103020266,
  • CRDB 01J1328947802,
  • NMB 20310008081,
  • AZANIA 00100021049

 

Jinsi ya Kujiunga na  Akiba ya Afya

  1. Bofya hapa, jaza fomu itakayotokea, pakua .PDF dokumenti, kisha itume kwenye barua pepe ya Chama (This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.)