Akaunti ya Akiba ya ELIMU inamuwezesha mwanachama kuchangia kwa hiari yake mwenyewe ili kukidhi mahitaji ya kulipa karo za shule/chuo kwa ajili yake, ndugu au wategemezi wake.
FAIDA ZA AKAUNTI YA AKIBA YA ELIMU
- Akiba itazaa faida ya Riba Juu ya Akiba (Interest on Savings) kila Mwaka
- Akiba ya Elimu inakuwezesha kupata Mkopo wa Elimu ambao ni mara mbili (2) ya Akiba ya Elimu
- Unaweza kupunguza Akiba ya Elimu mara nne(4) kwa mwaka (Kila robo mwaka mara moja) ikiwa fedha inayopunguzwa haiathiri dhamana ya Mkopo wa Elimu.
- Malipo hufanyika ndani ya masaa 24 endapo mwanachama akitaka kupunguza kiasi cha Akiba ya Elimu kwa njia ya Simu au Benki.
- Mwanachama anaweza kuchangia katika Akaunti hii kila anapopata fedha (Kwa njia ya Mshahara au Kuweka fedha katika akaunti za chama au Makubaliano ya Bank Standing Order).
VIGEZO NA MASHARTI
- Kiwango cha chini cha kuweka ni TZS. 50,000
AKAUNTI ZA BENKI ZA CHAMA
Jina la Akaunti ni: TRA SACCOS LTD:
- NBC 012103020266,
- CRDB 01J1328947802,
- NMB 20310008081,
- AZANIA 00100021049
JINSI YA KUFUNGUA AKAUNTI YA AKIBA YA ELIMU