1.0 Mkopo wa Week-End (Mkopo kwa Sekunde)

Mkopo wa Weekend unapatikana kwa njia ya mtandao muda wote/masaa ishirini na nne. Mkopo huu una sifa zifuatazo:

 1. Mwanachama anapata mkopo ndani ya Sekunde baada ya kufanya maombi
 2. Kiwango cha juu cha mkopo ni TSH 200,000.00
 3. Riba ya mkopo ni asilimia tano (5%); Mfano: kama mwanachama ameomba shilingi laki mbili, atalipa TSH 210,000.00
 4. Muda wa marejesho hautazidi siku therathini (30) baada ya kuomba mkopo.
 5. Mkopo huu hauhitaji dhamana yeyote
 6. Mwanachama atalazimika kulipa adhabu ya asilimia tano (5%) kwa kila mwezi anaochelewesha malipo

Mkopo huu unapatikana kwa mitandao yote ikiwa ni pamoja na M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, Ezy Pesa, T-Pesa, Hallo-Pesa.

 

1.2 Vigezo na Masharti

 1. Mwanachama atakaepitiliza muda wa marejesho (Siku 30) atapata adhabu ikiwa ni pamoja na kufungiwa kutumia huduma hii kwa muda wa miezi mitatu.
 2. Mwanachama hataweza kupata mkopo mpya endapo bado ana deni la mkopo huu
 3. Hakikisha unabadilisha nywila yako (Password)

 

1.3 Kujiunga na Huduma za mtandaoni

Ili mwanachama aweze kuomba mkopo huu atatakiwa kujiunga na huduma za mtandaoni kwa kufuata utaratibu ufuatao:

 1. Mwanachama ataomba kuwezeshwa kujiunga na huduma za mtandaoni kwa kujaza fomu na. TRAS/ICT/19/01 (Request for Online Services Form) ambayo ipo kwenye tovuti yetu.
 2. Idara ya TEHAMA itafanyia kazi maombi haya ndani ya masaa 12 na kumtumia mwanachama taarifa za siri katika simu yake (SMS)
 3. Mwanachama atatakiwa kutuma fomu hii kwa kutumia email yake ya TRA    (…@tra.go.tz) to This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

 

 

2.0 Jinsi ya Kupata Mkopo

Mwanachama akiishatumiwa taarifa za siri kwa njia ya ujumbe mfupi kwenye simu yake anaweza kuomba mkopo huu muda wowote.

 

2.1 Kwa njia ya mtandao

 • Bofya maneno haya, itafunguka fomu ya kuingiza taarifa za siri
 • Ingiza E-mail yako ya TRA kama Jina la Mtumiaji (User name) na nywila uliyotumiwa kwa njia ya Ujumbe Mfupi wa Simu kama ni mara ya kwanza au Ingiza uliyo badilisha
 • Chagua Weekend Loan, Ingiza kiasi unachohitaji kisha indinisha; muda huo huo fedha itaingiza katika Simu yako.

 

2.2 Kwa njia ya USSD

 • Piga *150*97%; kama umepiga namba hii kwa mara ya kwanza itakuhitaji kutengeneza password ya tarakimu nne
 • Ukiisha tengeneza password piga *150*97# ili uweze kukopa
 • Chagua Weekend-Loan, kisha idhinisha. Muda huo huo fedha itaingia katika simu yako.

 

3.0 Jinsi ya Kulipa

Malipo yanafanyika kwa njia ya mitandao ya simu ikiwa ni pamoja na M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, Ezy Pesa, T-Pesa, Hallo-Pesa.

Jinsi ya kulipa ni kama ifuatavyo:

TIGO PESA VODACOM (M-PESA) AIRTEL (AIRTEL MONEY)
 1. Piga *150*01#
 2. Chagua na. 7 "Huduma za kifedha"
 3. Chagua na. 1 "Tigo Pesa kwenda Benki"
 4. Chagua na. 11 "Benki Nyinginezo"
 5. Chagua na. 7 "GT"
 6. Chagua na. 1 "Kuingiza namba ya kumbukumbu"
 7. Ingiza namba yako ya kumbukumbu unayotumia kulog in. mfano: 100013209791(2).

 

Kumbuka: Namba ya mwisho weka 2 badala ya 1

Kumbuka: Wakati wa malipo kumbuka kuongeza riba ya 5% ya kiasi ulichokopa

Hatua ya mwisho ni kuweka namba ya siri ya TIGO-PESA

 1. Piga *150*00#
 2. Chagua na. 6 "Huduma za kifedha"
 3. Chagua na. 2 "M-Pesa kwenda Benki"
 4. Chagua na. 7 "G-L"
 5. Chagua na. 2 "GT"
 6. Chagua na. 1 "Kuingiza namba ya kumbukumbu"
 7. Ingiza Account namba yako unayotumia kulog in. mfano: 100013209791(2).

 

Kumbuka: Namba ya mwisho weka 2 badala ya 1

Kumbuka: Wakati wa malipo kumbuka kuongeza riba ya 5% ya kiasi ulichokopa

Hatua ya mwisho ni kuweka namba ya siri ya M-PESA

 1. Piga *150*60#
 2. Chagua na. 6 "Huduma za kifedha"
 3. Chagua na. 5 "Tuma kwenda Benki"
 4. Chagua na. 36 "GT BANK"
 5. Ingiza namba yako ya kumbukumbu unayotumia kulog in. mfano: 100013209791(2).

 

Kumbuka: Namba ya mwisho weka 2 badala ya 1

Kumbuka: Wakati wa malipo kumbuka kuongeza riba ya 5% ya kiasi ulichokopa

Hatua ya mwisho ni kuweka namba ya siri ya Airtel-Money

 

Kumbuka: mwanachama anaweza kulipa fedha yote kwa mkupuo au kidogo ila tu asizidi muda wa siku therathini (30).