Akaunti ya Wekeza ni akaunti ya akiba ambayo inamuwezesha mwanachama kuendelea kuchangia kwa kuwekeza katika akaunti hiyo bila kutoa fedha kwa kipindi cha kuanzia Miaka mitatu (3).


FAIDA ZA WEKEZA AKAUNTI

 1. Ni fursa kwa mwanachama kuwekeza Fedha yake kwa kipindi maalum.
 2. Riba ya Asilimia Saba (7%) inalipwa kila Mwaka kama faida baada mwanachama kufikisha TZS.500,000.
 3. Mwanachama anaweza kuchagua kulipwa riba yake au kuendelea kuiwekeza katika akaunti yake ya wekeza (Chaguo la kwanza, Chama kitamuingizia Mwanachaba faida yake (Riba) katika akaunti yake ya WEKEZA.
 4. Muda wa uwekezaji ni miaka mitatu(3)
 5. Mwanachama anaweza kuamua kuhuisha kipindi kipya cha uwekezaji wa miaka mitatu mingine kila mwisho wa miaka mitatu ya kwanza.
 6. Mwanachama anaweza kuchangia katika Akaunti hii kila anapopata fedha (Kwa njia ya Mshahara au Kuweka fedha katika akaunti za chama au Makubaliano ya Bank Standing Order).
 7. Inaweza kutumika kama dhamana ya mkopo.

 

VIGEZO NA MASHARTI

 1. Ili Kupata faida ya asilimia 7% kila mwaka, mwanachama hataruhusiwa kuchukua fedha katika akaunti hii kwa muda wa miaka mitatu(3)
 2. Endapo mwanachama ataamua kuchukua kiasi cha fedha au fedha yote katika akunti hii, atapata riba ambayo ni nusu ya riba iliyopatikana mwaka/miaka iliyopita

 

AKAUNTI ZA BENKI ZA CHAMA

Jina la Akaunti ni: TRA SACCOS LTD:

 • NBC 012103020266,
 • CRDB 01J1328947802,
 • NMB 20310008081,
 • AZANIA 00100021049

 

JINSI YA KUFUNGUA AKAUNTI YA WEKEZA

 1. Bofya hapa, jaza fomu itakayotokea, pakua .PDF dokumenti, kisha itume kwenye barua pepe ya Chama (This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.)