1.0 Mkopo wa Weekend (Mkopo wa Sekunde)

Mkopo wa Weekend ni mkopo  unaopatikana mtandaoni muda wote (24/7) kwa wanachama wa TRA SACCOS. Mkopo huu umebuniwa ili kukupa fedha kwa haraka pale unapohitaji ili kutatua changamoto/mahitaji ya haraka.

Sifa za Mkopo wa Weekend

  • Mwanachama hupata mkopo ndani ya sekunde chache baada ya kufanya maombi

  • Kiwango cha juu cha mkopo: TZS 200,000.00

  • Riba ya mkopo ni 5%

    • Mfano: Ukikopa TZS 200,000, utalipa TZS 210,000

  • Muda wa marejesho ni hadi siku 30 tangu tarehe ya mkopo

  • Mkopo huu hauhitaji dhamana

  • Adhabu ya kuchelewesha malipo ni 5% kwa kila mwezi

  • Mkopo unapatikana kupitia:

    • Mobile Application – TRA SACCOS Kiganjani

    • USSD – *150*45#

    • Members Portal- (Internet Banking)

Pakua TRA SACCOS Kiganjani 

Inapatikana kwenye:
                           Get it on Google Play

                         


1.2 Vigezo na Masharti

  • Mwanachama atakayepitiliza muda wa marejesho (siku 30) atalipa adhabu ya 5% na kufungiwa kutumia huduma hii kwa miezi mitatu (3)

  • Mwanachama hataruhusiwa kupata mkopo mpya endapo:

    • Ana deni la Mkopo wa Weekend 

    • Amechelewesha marejesho au ku-default mkopo mwingine

    • Ana hisa chini ya TZS 1,000,000

  • Mabadiliko yoyote ya namba ya simu uliyowasilisha kwa SACCOS yaripotiwe mara moja ili kuepuka uvujaji wa taarifa zako za kifedha


1.3 Kujiunga na Huduma za Mtandaoni

Ili kuomba Mkopo wa Weekend, mwanachama anatakiwa kujiunga na huduma za mtandaoni kwa kufuata utaratibu ufuatao:

  1. Kujaza Fomu ya Kufungua Akaunti ya JIKIMU kwa ajili ya Kuunganishwa na Huduma za USSD (*150*45#) / TRA SACCOS Kiganjani

  2. Kwa Internet Banking, mwanachama atahuisha taarifa zake kupitia fomu ya huduma za mtandaoni inayopatikana kwenye tovuti ya TRA SACCOS

  3. Fomu ijazwe na kutumwa kupitia barua pepe: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

  4. Maombi yatafanyiwa kazi ndani ya masaa 12, na mwanachama atapokea taarifa za siri (credentials) kupitia SMS

  5. Mwanachama anatakiwa kubadilisha PIN kupitia:

    • USSD: *150*45#

    • Au kwa kusajili akaunti kwenye TRA SACCOS Kiganjani


2.0 Jinsi ya Kupata Mkopo

Baada ya kupokea taarifa za siri (credentials), mwanachama anaweza kuomba mkopo huu wakati wowote.


2.1 Kupitia Mobile App – TRA SACCOS Kiganjani

  1. Ingia (Login) kwenye TRA SACCOS Kiganjani

  2. Nenda kwenye Menu → Apply Application

  3. Chagua Loan Type: WEEKEND

  4. Weka kiasi unachohitaji

  5. Bonyeza REQUEST LOAN

 Muamala utafanyika papo hapo na fedha itaingia kwenye JIKIMU Akaunti yako

Matumizi ya Fedha

Baada ya fedha kuingia JIKIMU Akaunti, unaweza:

  • Kutoa kupitia M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, Ezy Pesa, T-Pesa, HaloPesa

  • Kutoa kupitia ATM za Umoja Switch (Cardless Withdrawal)

  • Kulipia huduma ndani ya Chama:

    • Hisa

    • Mikopo mingine

  • Malipo ya Bill Mbalimbali kama Maji, Umeme, SGR, TV n.k

2.2 Kupitia USSD

  1. Piga *150*45#

  2. Kama ni mara ya kwanza:

    • Tengeneza PIN ya tarakimu 4 baada ya kupokea credentials

  3. Ingia kwenye mfumo kwa PIN yako

  4. Chagua Weekend Loan

  5. Idhinisha maombi

 Fedha itaingia mara moja kwenye JIKIMU Akaunti yako na unaweza kuitumia kama ilivyoelekezwa hapo juu.


3.0 Jinsi ya Kulipa Mkopo wa Weekend

Malipo hufanyika kupitia JIKIMU Akaunti yako.

Hatua za Kulipa

  1. Tuma fedha kwenda JIKIMU Akaunti yako kutoka:

    • Mitandao ya simu (MNOs)

    • Benki

  2. Ingia kupitia:

    • USSD: *150*45#

    • Au TRA SACCOS Kiganjani

  3. Chagua TRANSFER → WEEKEND LOAN ACCOUNT

  4. Weka kiasi cha deni kinachodaiwa

Mfano:
Ulikopa TZS 200,000, utalipa TZS 210,000

Baada ya malipo:

  • Salio la WEEKEND LOAN Account litasoma 0.00

  • Akaunti ya mkopo itafungwa moja kwa moja

Endapo kutakuwa na changamoto yoyote, wasiliana na watendaji wa TRA SACCOS kwa msaada zaidi.


AKAUNTI ZA BENKI ZA CHAMA

Jina la Akaunti: TRA SACCOS LTD

  • NBC: 012103020266

  • CRDB: 01J1328947802

  • NMB: 20310008081

  • AZANIA: 00100021049