MKOPO WA SIKUKUU (SIKUKUU LOAN)
1.0 Utangulizi
Mkopo wa Sikukuu ni huduma maalum ya kifedha inayotolewa na TRA SACCOS LTD kwa wanachama wake wakati wa msimu wa sikukuu. Mkopo huu unapatikana kwa njia ya mtandao ndani ya siku saba kabla ya sikukuu husika, kwa lengo la kuwasaidia wanachama kukidhi mahitaji yao muhimu kipindi cha sikukuu.
1.1 Sifa za Mkopo wa Sikukuu
Mkopo wa Sikukuu una sifa zifuatazo:
-
Hutolewa wakati wa sikukuu pekee kama vile Krismasi, Pasaka, Idd, Mwaka Mpya na sikukuu nyingine rasmi
-
Hautegemei akiba wala hauna dhamana
-
Unapatikana kupitia njia zifuatazo:
-
Mobile Application ya TRA SACCOS Kiganjani
-
USSD *150*45#
-
Internet Banking (Self Service)
-
-
Unawahusu wanachama waliokamilisha Fomu ya Kufungua Akaunti ya JIKIMU
-
Kiwango cha juu cha mkopo ni TZS 500,000
-
Muda wa marejesho ni miezi 3
-
Riba ni 3% (Reducing Balance)
-
Mwanachama aliye kwenye orodha ya wadaiwa (Defaulter) hatastahili mkopo huu
-
Mwanachama anatakiwa kuhakikisha taarifa zake za mawasiliano, hususan namba ya simu, ziko sahihi na zinaripotiwa mapema endapo zitabadilika, kwa ajili ya usalama wa taarifa zake za kifedha
1.2 Vigezo na Masharti
Masharti ya Mkopo wa Sikukuu ni kama ifuatavyo:
-
Mwanachama atakayeshindwa kulipa mkopo ndani ya muda wa miezi 3:
-
Atatozwa adhabu ya 5%
-
Atazuiwa kutumia huduma ya Mkopo wa Sikukuu kwa kipindi cha miezi mitatu
-
-
Mwanachama hataruhusiwa kupata mkopo mpya endapo:
-
Bado ana deni la Mkopo wa Sikukuu
-
Ame-default mkopo mwingine wowote ndani ya chama
-
Ana hisa pungufu ya TZS 1,000,000
-
-
Mabadiliko yoyote ya namba ya simu iliyowasilishwa kwa SACCOS yaripotiwe mara moja ili kuepuka uvujaji wa taarifa za kifedha
1.3 Kujiunga na Huduma za Mtandaoni
Ili mwanachama aweze kuomba Mkopo wa Sikukuu, anatakiwa kujiunga na huduma za mtandaoni kwa kufuata hatua zifuatazo:
-
Kujaza Fomu ya Kufungua Akaunti ya JIKIMU, inayopatikana kwenye tovuti ya TRA SACCOS
-
Kutuma fomu hiyo iliyojazwa kwenda barua pepe:
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. -
Maombi yatafanyiwa kazi ndani ya masaa 12
-
Mwanachama atapokea taarifa za siri za kuanzia (Credentials) kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS)
-
Mwanachama atatakiwa kubadilisha PIN mara moja kupitia:
-
USSD *150*45#, au
-
Mobile Application ya TRA SACCOS Kiganjani
-
2.0 Jinsi ya Kuomba Mkopo wa Sikukuu
Baada ya kupokea taarifa za siri, mwanachama anaweza kuomba Mkopo wa Sikukuu muda wowote wakati wa dirisha la sikukuu lililotangazwa.
2.1 Kuomba Mkopo Kupitia Mobile Application
Mwanachama atatakiwa kufuata hatua zifuatazo:
-
Kuingia (Login) kwenye TRA SACCOS Kiganjani baada ya kubadilisha PIN
-
Kuchagua Menu → Apply Application
-
Kuchagua Loan Type: SIKUKUU
-
Kuingiza kiasi cha mkopo kinachohitajika
-
Kubofya REQUEST LOAN
Baada ya ombi kufanyiwa kazi, fedha itawekwa kwenye JIKIMU Akaunti ya mwanachama.
Fedha hiyo inaweza kutumika kwa:
-
Kutoa kupitia mitandao ya simu (M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, Ezy Pesa, T-Pesa, Halo-Pesa)
-
Kutoa kupitia ATM za Umoja Switch (Cardless Withdrawal)
-
Kulipia hisa, mikopo mingine, au malipo ya huduma mbalimbali kama maji, umeme, SGR, TV na huduma nyingine ndani ya chama
2.2 Kuomba Mkopo Kupitia USSD
Hatua za kuomba mkopo kwa njia ya USSD ni kama ifuatavyo:
-
Piga *150*45#
-
Endapo ni matumizi ya mara ya kwanza, tengeneza PIN ya tarakimu 4 baada ya kupokea credentials
-
Ingia tena kwa kupiga *150*45#
-
Fuata maelekezo kwenye simu
-
Chagua Sikukuu Loan
-
Thibitisha ombi
Fedha itaingia moja kwa moja kwenye JIKIMU Akaunti ya mwanachama.
3.0 Jinsi ya Kulipa Mkopo wa Sikukuu
Malipo ya Mkopo wa Sikukuu hufanyika kupitia JIKIMU Akaunti ya mwanachama kwa utaratibu ufuatao:
-
Ingiza fedha kwenye JIKIMU Akaunti kupitia mitandao ya simu au benki
-
Ingia kwenye:
-
USSD *150*45#, au
-
Mobile Application ya TRA SACCOS Kiganjani
-
-
Chagua TRANSFER
-
Hamisha fedha kwenda SIKUKUU LOAN ACCOUNT
-
Weka kiasi cha deni kinachodaiwa
-
Thibitisha muamala kwa kubonyeza SEND MONEY
Baada ya mkopo kulipwa kikamilifu:
-
Salio la Akaunti ya Mkopo wa Sikukuu litasoma 0.00
-
Akaunti ya mkopo itafungwa rasmi
Endapo kutatokea changamoto yoyote, mwanachama anashauriwa kuwasiliana na watendaji wa TRA SACCOS kwa msaada zaidi.
4.0 Akaunti za Benki za Chama
Jina la Akaunti: TRA SACCOS LTD
-
NBC: 012103020266
-
CRDB: 01J1328947802
-
NMB: 20310008081
-
AZANIA BANK: 00100021049

