
TRA SACCOS LTD is a registered Savings and Credit Co-operative Society whose main objective is to mobilize savings from members and in return provide credit facilities. TRA SACCOS LTD is an employee-based SACCOS which was established under the current governing Co-operative Societies ACT No 20 of 2003 in 2006 and Licensed as Class B under microfinance act No 10 of 2018 in 2021. Other objectives of the SACCOS are to encourage thrift among its members by educating the members the advantages of developing a savings behavior, through proper investment best practices aimed at improving the social and economic conditions of the members. This is achieved by offering the members complementary savings schemes, credit facilities and other financial products as may be required by the members from time to time.
Jina la Akaunti ni: TRA SACCOS LTD:
Mkopo wa Weekend ni mkopo unaopatikana mtandaoni muda wote (24/7) kwa wanachama wa TRA SACCOS. Mkopo huu umebuniwa ili kukupa fedha kwa haraka pale unapohitaji ili kutatua changamoto/mahitaji ya haraka.
Mwanachama hupata mkopo ndani ya sekunde chache baada ya kufanya maombi
Kiwango cha juu cha mkopo: TZS 200,000.00
Riba ya mkopo ni 5%
Mfano: Ukikopa TZS 200,000, utalipa TZS 210,000
Muda wa marejesho ni hadi siku 30 tangu tarehe ya mkopo
Mkopo huu hauhitaji dhamana
Adhabu ya kuchelewesha malipo ni 5% kwa kila mwezi
Mkopo unapatikana kupitia:
Mobile Application – TRA SACCOS Kiganjani
USSD – *150*45#
Members Portal- (Internet Banking)
Mwanachama atakayepitiliza muda wa marejesho (siku 30) atalipa adhabu ya 5% na kufungiwa kutumia huduma hii kwa miezi mitatu (3)
Mwanachama hataruhusiwa kupata mkopo mpya endapo:
Ana deni la Mkopo wa Weekend
Amechelewesha marejesho au ku-default mkopo mwingine
Ana hisa chini ya TZS 1,000,000
Mabadiliko yoyote ya namba ya simu uliyowasilisha kwa SACCOS yaripotiwe mara moja ili kuepuka uvujaji wa taarifa zako za kifedha
Ili kuomba Mkopo wa Weekend, mwanachama anatakiwa kujiunga na huduma za mtandaoni kwa kufuata utaratibu ufuatao:
Kujaza Fomu ya Kufungua Akaunti ya JIKIMU kwa ajili ya Kuunganishwa na Huduma za USSD (*150*45#) / TRA SACCOS Kiganjani
Kwa Internet Banking, mwanachama atahuisha taarifa zake kupitia fomu ya huduma za mtandaoni inayopatikana kwenye tovuti ya TRA SACCOS
Fomu ijazwe na kutumwa kupitia barua pepe:
Maombi yatafanyiwa kazi ndani ya masaa 12, na mwanachama atapokea taarifa za siri (credentials) kupitia SMS
Mwanachama anatakiwa kubadilisha PIN kupitia:
USSD: *150*45#
Au kwa kusajili akaunti kwenye TRA SACCOS Kiganjani
Baada ya kupokea taarifa za siri (credentials), mwanachama anaweza kuomba mkopo huu wakati wowote.
Ingia (Login) kwenye TRA SACCOS Kiganjani
Nenda kwenye Menu → Apply Application
Chagua Loan Type: WEEKEND
Weka kiasi unachohitaji
Bonyeza REQUEST LOAN
Muamala utafanyika papo hapo na fedha itaingia kwenye JIKIMU Akaunti yako
Baada ya fedha kuingia JIKIMU Akaunti, unaweza:
Kutoa kupitia M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, Ezy Pesa, T-Pesa, HaloPesa
Kutoa kupitia ATM za Umoja Switch (Cardless Withdrawal)
Kulipia huduma ndani ya Chama:
Hisa
Mikopo mingine
Piga *150*45#
Kama ni mara ya kwanza:
Tengeneza PIN ya tarakimu 4 baada ya kupokea credentials
Ingia kwenye mfumo kwa PIN yako
Chagua Weekend Loan
Idhinisha maombi
Fedha itaingia mara moja kwenye JIKIMU Akaunti yako na unaweza kuitumia kama ilivyoelekezwa hapo juu.
Malipo hufanyika kupitia JIKIMU Akaunti yako.
Tuma fedha kwenda JIKIMU Akaunti yako kutoka:
Mitandao ya simu (MNOs)
Benki
Ingia kupitia:
USSD: *150*45#
Au TRA SACCOS Kiganjani
Chagua TRANSFER → WEEKEND LOAN ACCOUNT
Weka kiasi cha deni kinachodaiwa
Mfano:
Ulikopa TZS 200,000, utalipa TZS 210,000
Baada ya malipo:
Salio la WEEKEND LOAN Account litasoma 0.00
Akaunti ya mkopo itafungwa moja kwa moja
Endapo kutakuwa na changamoto yoyote, wasiliana na watendaji wa TRA SACCOS kwa msaada zaidi.
Jina la Akaunti: TRA SACCOS LTD
NBC: 012103020266
CRDB: 01J1328947802
NMB: 20310008081
AZANIA: 00100021049
Mkopo wa Sikukuu ni huduma maalum ya kifedha inayotolewa na TRA SACCOS LTD kwa wanachama wake wakati wa msimu wa sikukuu. Mkopo huu unapatikana kwa njia ya mtandao ndani ya siku saba kabla ya sikukuu husika, kwa lengo la kuwasaidia wanachama kukidhi mahitaji yao muhimu kipindi cha sikukuu.
Mkopo wa Sikukuu una sifa zifuatazo:
Hutolewa wakati wa sikukuu pekee kama vile Krismasi, Pasaka, Idd, Mwaka Mpya na sikukuu nyingine rasmi
Hautegemei akiba wala hauna dhamana
Unapatikana kupitia njia zifuatazo:
Mobile Application ya TRA SACCOS Kiganjani
USSD *150*45#
Internet Banking (Self Service)
Unawahusu wanachama waliokamilisha Fomu ya Kufungua Akaunti ya JIKIMU
Kiwango cha juu cha mkopo ni TZS 500,000
Muda wa marejesho ni miezi 3
Riba ni 3% (Reducing Balance)
Mwanachama aliye kwenye orodha ya wadaiwa (Defaulter) hatastahili mkopo huu
Mwanachama anatakiwa kuhakikisha taarifa zake za mawasiliano, hususan namba ya simu, ziko sahihi na zinaripotiwa mapema endapo zitabadilika, kwa ajili ya usalama wa taarifa zake za kifedha
Masharti ya Mkopo wa Sikukuu ni kama ifuatavyo:
Mwanachama atakayeshindwa kulipa mkopo ndani ya muda wa miezi 3:
Atatozwa adhabu ya 5%
Atazuiwa kutumia huduma ya Mkopo wa Sikukuu kwa kipindi cha miezi mitatu
Mwanachama hataruhusiwa kupata mkopo mpya endapo:
Bado ana deni la Mkopo wa Sikukuu
Ame-default mkopo mwingine wowote ndani ya chama
Ana hisa pungufu ya TZS 1,000,000
Mabadiliko yoyote ya namba ya simu iliyowasilishwa kwa SACCOS yaripotiwe mara moja ili kuepuka uvujaji wa taarifa za kifedha
Ili mwanachama aweze kuomba Mkopo wa Sikukuu, anatakiwa kujiunga na huduma za mtandaoni kwa kufuata hatua zifuatazo:
Kujaza Fomu ya Kufungua Akaunti ya JIKIMU, inayopatikana kwenye tovuti ya TRA SACCOS
Kutuma fomu hiyo iliyojazwa kwenda barua pepe:
Maombi yatafanyiwa kazi ndani ya masaa 12
Mwanachama atapokea taarifa za siri za kuanzia (Credentials) kupitia ujumbe mfupi wa simu (SMS)
Mwanachama atatakiwa kubadilisha PIN mara moja kupitia:
USSD *150*45#, au
Mobile Application ya TRA SACCOS Kiganjani
Baada ya kupokea taarifa za siri, mwanachama anaweza kuomba Mkopo wa Sikukuu muda wowote wakati wa dirisha la sikukuu lililotangazwa.
Mwanachama atatakiwa kufuata hatua zifuatazo:
Kuingia (Login) kwenye TRA SACCOS Kiganjani baada ya kubadilisha PIN
Kuchagua Menu → Apply Application
Kuchagua Loan Type: SIKUKUU
Kuingiza kiasi cha mkopo kinachohitajika
Kubofya REQUEST LOAN
Baada ya ombi kufanyiwa kazi, fedha itawekwa kwenye JIKIMU Akaunti ya mwanachama.
Fedha hiyo inaweza kutumika kwa:
Kutoa kupitia mitandao ya simu (M-Pesa, Airtel Money, Tigo Pesa, Ezy Pesa, T-Pesa, Halo-Pesa)
Kutoa kupitia ATM za Umoja Switch (Cardless Withdrawal)
Kulipia hisa, mikopo mingine, au malipo ya huduma mbalimbali kama maji, umeme, SGR, TV na huduma nyingine ndani ya chama
Hatua za kuomba mkopo kwa njia ya USSD ni kama ifuatavyo:
Piga *150*45#
Endapo ni matumizi ya mara ya kwanza, tengeneza PIN ya tarakimu 4 baada ya kupokea credentials
Ingia tena kwa kupiga *150*45#
Fuata maelekezo kwenye simu
Chagua Sikukuu Loan
Thibitisha ombi
Fedha itaingia moja kwa moja kwenye JIKIMU Akaunti ya mwanachama.
Malipo ya Mkopo wa Sikukuu hufanyika kupitia JIKIMU Akaunti ya mwanachama kwa utaratibu ufuatao:
Ingiza fedha kwenye JIKIMU Akaunti kupitia mitandao ya simu au benki
Ingia kwenye:
USSD *150*45#, au
Mobile Application ya TRA SACCOS Kiganjani
Chagua TRANSFER
Hamisha fedha kwenda SIKUKUU LOAN ACCOUNT
Weka kiasi cha deni kinachodaiwa
Thibitisha muamala kwa kubonyeza SEND MONEY
Baada ya mkopo kulipwa kikamilifu:
Salio la Akaunti ya Mkopo wa Sikukuu litasoma 0.00
Akaunti ya mkopo itafungwa rasmi
Endapo kutatokea changamoto yoyote, mwanachama anashauriwa kuwasiliana na watendaji wa TRA SACCOS kwa msaada zaidi.
Jina la Akaunti: TRA SACCOS LTD
NBC: 012103020266
CRDB: 01J1328947802
NMB: 20310008081
AZANIA BANK: 00100021049
TRA SACCOS LTD INAWAKARIBISHA WANACHAMA WOTE WA VITUO VYA DAR ES SALAAM KWENYE MKUTANO WA MAANDALIZI YA AGM 2025:
Ndugu Mwanachama,
Kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wetu, Mkutano wa Vituo vya DSM uliopaswa kufanyika wikiendi iliyopita ya tarehe 1 & 2 Novemba, sasa utafanyika siku ya Jumamosi na Jumapili, tarehe 8 na 9 Novemba 2025.
Mahali: Katika Ukumbi wa Multipurpose Hall - Chuo cha Kodi (ITA) -Mikocheni Industraial Area
Muda:Kuanzia saa 1:30 asubuhi, kwa kuzingatia mgawanyo wa vituo wa awali.
RATIBA YA VITUO:
| Wataohudhuria Tarehe 8: | Wataohudhuria Tarehe 9: |
|
LTD HQ,ICDS,KINONDONI,ILALA I,ILALA II,KARIAKOO,HQ-I,HQ-II ,TEMEKE,DRD HQ,ICT |
WHARF ,CSC ,FAST TMU, HQ-III ,HQ-IV, JNIA, PCA, SCANNER, TEGETA, CSC-HQ, ITA, MTD HQ, CSC-MAFUTA, BUGURUNI, OUT OF TRA, RETIRED TRA, TRA IN KENYA and TRANSFERRED MANZESE UPANGA KIMARA |
CHA KUZINGATIA:
Tafadhali hakikisha unahudhuria, kwani huu ni Mkutano muhimu kwa maendeleo ya Chama Chetu. Usisahau kitambulisho cha kazi kwa ajili ya usajili.
Ratiba:
|
MUDA |
DAKIKA |
TUKIO/MADA |
MHUSIKA |
|
01:30 – 03:00 Asubuhi |
90 |
KUJIANDIKISHA NA KUINGIA UKUMBINI |
WOTE |
|
03:00 – 03:10 Asubuhi |
10 |
SALA/DUA |
MJUMBE ALIYECHAGULIWA |
|
03:10 – 03:30 Asubuhi |
20 |
UTAMBULISHO NA SALAMU ZA UKARIBISHO. |
MWENYEKITI |
|
03:30 - 4:30 Asubuhi |
60 |
UWASILISHAJI WA BAJETI YA MWAKA 2026 |
MENEJA |
|
04:30 - 5:00 Asubuhi |
30 |
UWASILISHAJI WA MAPENDEKEZO YA BIDHAA NA KUFUNGUA FUNGAMANO |
MENEJA |
|
05:00 - 05:45 Asubuhi |
45 |
MAPUMZIKO YA CHAI |
WOTE |
|
05:45 Asubuhi – 06:20 Mchana |
35 |
MJADALA |
WOTE |
|
06:20 – 06:30 Mchana |
|
SALA/DUA |
MJUMBE ALIYECHAGULIWA |
Karibu sana!